|
Wajumbe wa Baraza ni nani na wamechaguliwaje? |
|
|
|
|
Mkutano wa kwanza uliidinisha muundo wa Baraza ili kuongoza uundaji wa mkutano wa mwafaka wa wawekezaji kama kamati yake tendaji ya kwanza. Mikutano minne tayari imeshafanyika chini ya Uenyekiti wa Mheshimiwa Rais Benjamini William Mkapa.
Mikutano ya Mwafaka na wawekezaji inaweka watu maarufu pamoja; wa Kimataifa na wawekezaji wa ndani katika majadiliano ya mwafaka pamoja na Rais na Baraza la Mawaziri katika mawazo na vitendo katika kuifanya nchi iwe mahali pa uwekezaji katika kanda.
Kuendeleza mazungumzo ya "win-win' kwa ajili ya maendeleo, mfumo wa ubia wa SMART umeanzishwa, na TNBC imeteuliwa kusimamia mchakato kama kitovu cha shughuli. Kamati tendaji ya Ubia wa SMART kwa sasa unaundwa na lengo lake ni kuingia katika mazungumzo ya ndani kuanzia kwenye wilaya hadi kwenye mkoa na katika ngazi ya Taifa katika kuandaa kwa ajili ya kuwa wenyeji wa mazungumzo ya Kimataifa katika siku za hivi karibuni.
Mpango unaofadhiliwa na wabia wa maendeleo unaolenga katika kuongoza mchakato wa mabadiliko na kuboresha mazingira ya biashara umezinduliwa.
BEST inalenga kuhusu uboreshaji wa mazingira ya kisheria unachunguza sheria na kanuni mbalimbali zinazoathiri biashara, inatazama utaratibu wa masuluhisho ya kibiashara, kubadili mawazo ya utumishi, kuimarisha kituo cha Uwekezaji cha Tanzania (TIC) ambacho ni muhimu katika uwekezaji wa kuendeleza uraghibishaji wa sekta binafsi.
Baraza limepewa wajibu wa kusimamia na kutathmini BEST na kuanzisha Kamati tendaji yenye kufanya kazi kwa dhati.
Mwelekeo wa dunia ya sasa umeanzisha fursa na changamoto kwa serikali na wabia katika nchi zilizoendelea na zinazoendelea. Utandawazi wa shughuli za kiuchumi, Biashara huria na ushindani mkali ambao umeonyeshwa na makampuni ya ndani, utendaji mbaya wa mashirika yanayomilikiwa na serikali na matokeo yanayotokana na maslahi katika nafasi ya sekta binafsi katika uzalishaji wa mali ya taifa vimeungana katika kuzisukuma serikali za Afrika kutafuta modeli mpya za usimamizi wa uchumi.
Katika Tanzania, serikali imeingia katika zoezi muhimu la marekebisho yenye lengo la kuiweka nchi mahali ambapo itakuwa na uwezo wa kuogelea katika mwelekeo wa uchumi wa dunia unaoibuka. Kwa muda mrefu serikali imetambua kuwa ukuaji wa uchumi hatimaye hutegemea nguvu za Sekta Binafsi. Uwezo wake wa kutatua matatizo kama vile uondoaji wa umaskini, uanzishwaji ajira na ustawi wa watu kwa ujumla pia ukuaji wa uchumi wa Sekta binafsi iliyo imara huiongezea serikali mapato.
|